- Vikki Thompson na Alan Thomas Kennedy-Asser, Chuo Kikuu cha Bristol
Joto kali nchini India na Pakistani limewaacha zaidi ya watu bilioni moja katika sehemu yenye watu wengi zaidi duniani wakikabiliwa na halijoto ya zaidi ya 40℃. Ingawa hii haijavunja rekodi za wakati wote kwa mikoa, sehemu yenye joto zaidi ya mwaka bado inakuja.